Exodus 24:12-17

12 a Bwana akamwambia Musa, “Panda uje kwangu huku mlimani na ukae hapa, nami nitakupa vibao vya mawe, vyenye sheria na amri ambazo nimeziandika ziwe mwongozo wao.”

13 bBasi Musa akaondoka na Yoshua mtumishi wake, naye Musa akapanda juu kwenye mlima wa Mungu. 14 cMusa akawaambia wazee wa Israeli, “Tungojeni hapa mpaka tutakapowarudia. Haruni na Huri wako pamoja nanyi, na kila aliye na neno aweza kuwaendea wao.”

15 dMusa alipopanda juu mlimani, wingu liliufunika huo mlima, 16 enao utukufu wa Bwana ukatua juu ya Mlima Sinai. Kwa muda wa siku sita wingu lilifunika mlima, na siku ya saba Bwana akamwita Musa kutoka katikati ya lile wingu. 17 fKwa Waisraeli utukufu wa Bwana ulionekana kama moto uteketezao juu ya mlima.
Copyright information for SwhKC